Monday, June 18, 2012

MWAKALEBELA AKUNWA NA UJUMBE WA NAPE

 
NA mcdonald masse-Iringa
ALIYEKUWA mshindi wa kura za maoni ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) katika kinyang'anyiro cha kumsaka mgombea ubunge wa CCM jimbo la Iringa mjini mwaka 2010 Frederick Mwakalebela ameeleza kufurahishwa na kauli ya katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye kuhusu ukweli wa mbunge Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) kupita katika uchaguzi huo.

Hivyo awataka vijana wa kuacha kukimbilia vyama vya upinzani na badala yake kuendelea kutulia ndani ya CCM kwa madai kuwa kuna mikakati kambambe anayoifanya kwa ajili ya kuwawezesha vijana hao ili kuwa wajasiriamali badala ya kushinda vijiweni .
Alisema kuwa kuwa uwazi na ukweli wa Nape kuhusu makosa yaliyojitokeza katika jimbo hilo la Iringa mjini ni moja kati ya mambo ambayo wananchi wa jimbo la Iringa mjini walitegemea kuelezwa na kiongozi huyo .

Hivyo alisema kuwa mbali ya kuwa bado hajaamua kugombea ama kutogombea katika jimbo hilo ila bado ataendelea kuwa kada mzuri wa CCM na wala hatajaribu kukihama chama chake CCM kama ambavyo baadhi ya makada wenzake wanavyofanya.

" Napenda kumpongeza sana katibu wangu wa itikadi na uenezi Taifa Nape Nnauye kwa kuwaeleza ukweli wapiga kura wa jimbo la Iringa mjini ambao baadhi yao walikuwa wakirubuniwa na vyama vya upinzani kuwa labda CCM haitaweka ukweli wa kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi mkuu mwaka 2010.....nataka vijana wa jimbo la Iringa mjini watambue kuwa mimi bado ni mwana CCM na nitaendelea kuwa karibu na chama changu"

Mwakalebela alitoa kauli hiyo leo alipozungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kwa njia ya simu kuhusiana na msimamo wake kisiasa na maoni yake juu ya vijana wanaoendelea kushabikia upinzani kama njia ya kuchukizwa na hatua ya CCM mwaka 2010 kuengua jina la Mwakalebela.

Alisema kuwa ni vema vijana kutambua kuwa CCM ndicho chama chenye mwelekeo wa kuwatumikia wananchi na kuwa ni vema vijana hao kuendelea kubanana ndani ya CCM badala ya kuhama chama hicho.

Akielezea kuhusu mikakati yake ya kuwasaidia vijana wa jimbo hilo la Iringa mjini Mwakalebela alisema kuwa bado anauchungu na vijana wa Iringa mjini na hivyo amejipanga kuwasaidia kuwaunganisha na vikundi vya ujasiria mali pamoja na kuendelea kuwaunganisha vijana hao bila kujali itikadi ya kisiasa katika michezo ambayo itaanza hivi karibuni.

Kwa upande wake baadhi ya vijana na wazee wa mjini Iringa wamepongeza ziara hiyo ya Nape mjini Iringa kuwa ni ziara iliyolenga kumaliza uongo wa uongozi wa viongozi wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) dhidi ya serikali ya CCM .

Alisema mzee Ambweni Kyando mkazi wa Mwangata katika Manispaa ya Iringa kuwa bado anashangazwa na baadhi ya waliokuwa wagombea katuka kura za maoni ubunge jimbo la Iringa mjini akiwemo Zuberi Mwachura kukimbilia upinzani wakati ni mmoja kati ya makada wazuri wa CCM waliotegemewa kuja kupewa nafasi za juu

Wednesday, June 13, 2012

                           Dk Mwakyembe awasha moto TRLBAADA ya kusafiri kwa treni kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amebaini hujuma nzito katika Shirika la Reli Tanzania (TRL) ikiwamo ofisa mmoja kuwaibia abiria kwa kughushi viwango vya nauli na ameagiza afukuzwe kazi.

Licha ya kuagiza kutimuliwa kwa ofisa huyo, pia alitangaza kuandaliwa utaratibu wa kufanya mabadiliko kadhaa katika kuboresha usafiri huo, ikiwamo kuondoa malipo ya nusu nauli kwa watoto wadogo kuanzia miaka mitatu hadi miaka 10 na pia kuondolewa kwa utaratibu wa malipo ya mizigo midogo ya abiria.

Juzi, Dk Mwakyembe ambaye tayari amewang’oa vigogo wanne wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), aliamua kusafiri kwa treni hadi Dodoma akitokea Dar es Salaam ili kujionea utendaji kazi wa shirika hilo.

Mara baada ya kuwasili katika Stesheni ya Dodoma saa 1:30 asubuhi, Waziri Mwakyembe alizungumza na waandishi wa habari na kusema akiwa katika safari hiyo, amepata fursa za kutembelea mabehewa yote na kuzungumza na abiria.

Dk Mwayembe alisema ingawa safari ilikuwa nzuri, kuna mengi ambayo ameyabaini ambayo ni pamoja na abiria kulipa nauli kubwa na kuandikiwa tiketi tofauti jambo ambalo alisema ni wizi na kamwe wizara yake haiwezi kulifumbia macho.

“Unakuta nauli halali ni Sh9,000 lakini, abiria ameandikiwa Sh29,000. Sasa nimeagiza huyu anayehusika afuatiliwe na kujulikana na nipewe taarifa ameondolewa,” aliagiza Dk Mwakyembe.
Alisema pia katika safari hiyo, alibaini uchakavu mkubwa wa mabehewa na hakuna tofauti ya daraja la tatu na la kwanza, upungufu mwingine ni katika utendaji na taratibu jambo ambalo linapaswa kuchukuliwa hatua.

Dk Mwakyembe alisema si vyema mtoto kuanzia miaka mitatu kulipishwa nusu nauli, kwani taratibu zinapaswa kufanywa ili hadi mtoto wa miaka 10 ikiwezekana asilipishwe nauli kwani treni ndiyo usafiri wa umma.

Kuhusu mizigo, alisema kwa sasa mizigo ya abiria inalipiwa kwa kilo kama ilivyo usafiri wa ndege jambo ambalo si sawa kwani mzigo wa abiria kuanzia kilo 20 unalipishwa jambo ambalo linapaswa kuangaliwa.

“Usafiri huu mimi nasema ndiyo wa umma hivyo, tusizuie watu kupeleka hata zawadi nyumbani kwao ni vyema tuwe na utaratibu walau mizigo kidogo ya abiria isilipiwe,” alisema Dk Mwakyembe.

Safari tatu kwa wiki
Akizungumzia tatizo la ratiba za usafiri, Dk Mwakyembe alisema mipango inafanywa ili kufikia Desemba, mwaka huu walau kuwe na safari tatu za kutoka Dar es Salaam hadi  Kigoma na Tabora na kuondoa kero zilizopo sasa.

Waziri huyo alisema anaamini safari hizo zikirejea, zitapunguza wingi wa abiria na msongamano wa watu kwenye treni na pia zitasaidia kuanza kwa usafirishaji wa mizigo kwa kutumia usafiri huo.
“Tutawaomba wabunge wapitishe bajeti yetu na wapande treni ili kuona usafiri huu, nina amani tukiondoa upungufu kidogo, huu utakuwa usafiri mzuri sana,” alisema.

Hujuma
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tzeba ambaye allimpokea Dk Mwakyembe alisema licha ya kuwepo hujuma katika nauli za abiria, pia wamebaini hujuma kubwa katika mizigo inayosafirishwa kwa reli katika mashirika yote ya TRC na Shirika la Tanzania na Zambia (Tazara).

Alisema maofisa wasio waadilifu wa mashirika hayo, wamekuwa wakisafirisha mizigo mingi lakini inayoandikiwa na kulipwa serikalini ni ile yenye uzito mdogo.

“Utakuta mzigo wa tani 40 hadi 60 unaandikiwa tani 10 au 20 fedha nyingine zinaingia mifukoni mwa wajanja, hatutakubali jambo hili,” alisema Dk Tzeba
Alisema yeye na waziri wake, pamoja na maofisa wengine, watakuwa wakisafiri kwa kushtukiza kwa reli mara kwa mara ili kubaini hujuma zote na kuwachukulia hatua wahusika mara moja.
“Mimi nilikuja hapa Dodoma kwa kiberenge na baadhi ya wabunge wa kamati ya miundombinu na leo amekuja waziri kwa treni hii haitakuwa mara yetu ya kwanza, tutasafiri sana kwa reli ili kubaini hujuma zilizopo,” alisema Dk Tzeba.

Tuesday, June 12, 2012

Tegete: Yanga imelamba dume kumsajili Yondani 


Tegete

 


MSHAMBULIAJI wa Yanga, Jerryson Tagete amesema kusajiliwa klabu hiyo ya Jangwani beki wa zamani wa Simba, Kelvin Yondan kutasaidia kufika mbali katika mashindano ya ndani na nje kutokana na uwezo mkubwa aliona mlinzi huyo.
Tegete aliyeongeza mkataba wa miaka miwili zaidi kuicheza Yanga, alisema ana imani kubwa na uwezo wa Yondani na kwamba uongozi wa Yanga hakufanya chaguo baya kumsajili.
 Mpachika mabao huyo wa Jangwani aliyepwaya msimu uliomalizika, amesema eye binafsi anafurahi kubaki Yanga na atakuwa tayari kuonyesha ushirikiano na beki wao mpya Yondani.
Akizungumza jana na kituo kimoja cha Radio, Tegete alisema kinachomfurahisha zaidi ni uwapo wa Yondani kwenye kikosi hicho kilichopoteza mwelekeo msimu uliopita na kumaliza ligi nafasi ya tatu ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka 20.
"Tathimini yangu ni kwamba, Yondani ni beki mzuri anayekubalika na wengi. Kweli nafarijika kuja kwake Jangwani nikiamini atakuwa msaada mkubwa," alisema Tegete aliyewahi kuhusishwa kutaka kuhamia Simba msimu ujao.
Kuhusu kuongezewa mkataba, Tegete alisema amefurahishwa na hatua ya viongozi wake kwa vile ana mapenzi ya dhati na klabu hiyo ya Jangwani, mabingwa wa sas Kombe la Kagame.
"Sikuwahi kuwa na mpango wa kuhama Yanga, lakini naweza kufanya hivyo iwapo tu nitapata klabu ya kucheza nchi ya Tanzania na siyo kinyume chake," alisema.
Wakati huohuo, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amewataka viongozi wa Yanga na Simba kutoendelea na utamaduni wa kupoteza muda kwa mambo yaliyokosa mashiko.
Kauli hiyo ametoa jana baada ya kuwepo na mvutano kati ya viongozi wa timu hizo mbili juu ya usajili wa beki wa Simba Kevin Yondani ambaye inadaiwa kuwa amesajiliwa na Yanga.
Alisema viongozi wa timu hizo mbili wote wanazifahamu taratibu za usajili hivyo kama kuna udanganyifu kila kitu kipo wazi hivyo wasipoteza muda kwa mambo yasiyokuwa ya msingi.
"Lazima kati ya pende hizo mbili kutakuwepo na mmoja ambaye ni muongo hivyo hakuna haja ya kupoteza muda wa kupigizana kelele kwa sababu kila kitu kipo wazi" alisema Tenga.

                         Ziara za Pinda zazua balaa bungeni                                                     Waziri Mkuu,Mizengo Pinda
MBUNGE wa Viti Maalumu (Chadema), Rose Kamili ameibua tuhuma nzito dhidi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, akisema mtendaji mmoja wa Serikali alikamatwa kutokana na kushindwa kukusanya mchango wa mbuzi tisa za zawadi kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati wa ziara yake Wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu.

Kamili alirusha kombora hilo, wakati akiuliza swali la nyongeza kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Aggrey Mwanri baada ya swali la msingi lililoulizwa na Mbunge wa Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbayi (Chadema), kuhusu mipaka ya madaraka kati ya Serikali za Mitaa na Serikali Kuu inaanzia na kuishia wapi kiutendaji.

Baada ya swali hilo la msingi, Kamili aliuliza swali la nyongeza akisema Mkuu wa Wilaya ya Maswa aliwaagiza watendaji wote wa kata kukusanya mbuzi ikiwa ni zawadi za ujio wa Waziri Mkuu katika wilaya yao walioshindwa walikamatwa.

Akijibu swali hilo, Mwanri alisema ofisi yake haina taarifa ya tuhuma hizo na kumtaka mbunge huyo azithibitishe. Alisema Serikali haina utaratibu wa kuomba kupewa zawadi mbalimbali kwa viongozi wake na kama mbunge huyo ana ushahidi wa suala hilo autoe.

Mara baada ya majibu hayo, Spika wa Bunge, Anne Makinda alimpa fursa mbunge huyo kueleza kama anao ushahidi huo na akajibu kuwa anao kwani aliona hata kupitia luninga Waziri Mkuu Pinda akikabidhiwa zawadi.

Hata hivyo, majibu hayo ya Kamili  yalionekana kutomridhisha Spika Makinda ambaye alisema taarifa za luninga haziwezi kuwa ushahidi na akawataka wabunge kuwa makini na taarifa wanazotoa bungeni.
Awali, Kamili aliulizia juu ya operesheni ya kuhamisha wakazi wa pori la Maswa ambao nyumba zao kadhaa zilichomwa moto na wafugaji kadhaa kutimuliwa bila kujua pa kwenda.

Akijibu swali hiyo, Mwanri alisema mgogoro huo wa kuhamishwa wananchi hao, tayari ulifuatiliwa na Serikali na Waziri wa Nchi, Tamisemi wakati huo, George Mkuchika alikwenda katika eneo hilo na kuzungumza na wananchi na kupata taarifa sahihi.

Hata hivyo, alisema wananchi wa vijiji saba vya eneo hilo, walikubaliana kuanzisha Hifadhi ya Jamii (WMA) na kutoa eneo hilo kwa mwekezaji jambo ambalo lilitekelezwa.

Awali, akijibu swali la Kasulumbayi, Naibu Waziri Mwanry alisema wakuu wa mikoa na wilaya nchini, hawaruhusiwi kwa mujibu wa sheria, kuingilia utendaji kazi wa mamlaka za Serikali za Mitaa, ikiwa zinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sera, sheria, kanuni na miongozo iliyowekwa na Serikali.


Kasulumbayi alitaka kujua inakuwaje wakuu wa mikoa na wilaya ambao kiutendaji ni watumishi wa Serikali Kuu, wanatoa amri kwa watendaji walio chini ya wakurugenzi wa wilaya, kuhamisha wananchi katika maeneo yao. Akahoji mpaka wa madaraka kati ya Serikali za Mitaa na Serikali Kuu unaanzia na kuishia wapi kiutendaji?

Mwanri alisema mkuu wa mkoa kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa Na.19 ya mwaka 1997, katika vifungu Na 5, 6 na 7 ana wajibu wa kusimamia kazi na shughuli zote za Serikali katika mkoa ikiwa  ni pamoja na kuziwezesha mamlaka za Serikali za Mitaa, kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizotungwa na Bunge.

Alisema majukumu ya wakuu wa wilaya yametengwa katika kifungu Na.14 (1-3) cha Sheria ya Tamisemi, Na.19 ya mwaka 1997 kwamba yeye ndiye msimamizi mkuu wa shughuli za Serikali katika wilaya yake.

“Hivyo madaraka ya jumla ya mkuu wa wilaya yanatiririshwa kutoka kwa Mheshimiwa Rais kupitia kwa mkuu wa mkoa, kwa upande wa watendaji walio chini ya mkurugenzi wa halmashauri, wao ni watekelezaji wa shughuli za Serikali kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo,” alisema.

Hata hivyo, alisema mipaka ya madaraka kati ya Serikali za Mitaa na Serikali Kuu imeanishwa katika Sheria za Mamlaka za Serikali za Mitaa na Sheria ya Tawala za Mikoa Na 19 ya 1997.

“Kwa kuzingatia sheria hizo ni kwamba mkuu wa mkoa na wilaya anaruhusiwa kuingilia kati inapotokea mamlaka za Serikali za Mitaa zimeshindwa kutekeleza majukumu yao au kukiuka misingi ya sera na sheria zilizopo.

Thursday, June 7, 2012

KAA TAYARI KWA UJIO WA KITUO KIPYA CHA REDIO KATIKA MJI WA MAKAMBAKO NDANI YA MKOA MPYA WA NJOMBE.

Tuesday, June 5, 2012

                                             Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa

 

Kawambwa kutangaza majina 100 wanaodhaminiwa MCL 

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kutangaza majina 100 ya wanafunzi watakaopata udhamini wa elimu.

Udhamini huo unatolewa chini ya mpango maalum wa kusaidia ukuaji wa elimu unaoendeshwa na Mwananchi Communications Limited (MCL) kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

MCL ndiyo inayochapisha magazeti ya mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti.
Ofisa Masoko wa MCL, Edward Uisso alisema jana kuwa mara baada ya Waziri  kuyatangaza majina hayo   yatachapishwa katika magazeti yote ya MCL kesho.

Uisso alisema mpango huo uliopewa jina la “Paa na Mwananchi” ulihusisha  watoto wa Kitanzania tu wanaosoma shule za umma kote nchini na utaanza mara moja kwa washindi waliochaguliwa.

“Harakati za ‘Paa na Mwananchi’ zinafikia mwisho baada ya kuanza  Aprili 2, mwaka huu na leo washindi watatangazwa ambao kesho majina yao yatachapishwa katika magazeti yote ya MCL,” alisema Uisso na kuongeza:

Mpango huu wa Paa na Mwananchi unafanyika katika nchi zote za Afrika Mashariki ambazo Kampuni ya Nation Media Group (NMG), ina matawi, huu ni mpango wa kutoa udhamini wa elimu kwa wananchi wote ambao hawana uwezo wa kusomesha watoto wao.

Uisso alisema udhamini huu utahusu karo yote ya shule, sare kwa mwanafunzi, vitabu, madaftari na mahitaji mengine muhimu ya mwanafunzi.

Watoto watakaopata ufadhili huu, kuna wakati watakuwa wanafanya ziara ya kimasomo  katika nchi za Afrika Mashariki, lengo likiwa ni kupata uelewa tofauti na kubadilisha mawazo na wenzao.

Uisso alisema kuwakutanisha na wenzao wa nchi za Afrika Mashariki ni  kuwajenga watoto kifikra ili waweze kuwa na uwezo wa kushindana na wenzao kutoka nchi za husika na nje ya ukanda huu.

“Katika ziara kutakuwa na wataalamu waliobobea katika taaluma mbalimbali watakaowapa mafunzo wanafunzi hao na wakati mwingine wataalamu hao watakuja hapa nchini kuwafundisha wakiwa hapa hapa,” alisema Uisso.

Friday, June 1, 2012
Wasanii maarufu wa Orijino Komedi na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ na bendi yake ya Machozi wanatarajiwa kutumika kutunisha mfuko utakaofanikisha Siku ya Utalii Duniani, ambayo kitaifa itafanyika mkoani hapa. Zaidi ya Sh milioni 120 zimekadiriwa kutumika kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe hiyo itakayofanyika kwa wiki nzima kuanzia Septemba 28 hadi Oktoba 4, mwaka huu.

Mratibu wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe hizo, Fidiah Nakamendu alisema jana kwenye kikao cha maandalizi kwamba sherehe hizo zitafanyika nje kidogo ya Manispaa ya Iringa katika Kijiji cha Nduli, karibu na Uwanja wa Ndege wa Nduli. Alisema wasanii hao watafanya maonyesho yao katika mabonanza yatakayoandaliwa baadaye mjini Iringa. Alitaja mikakati mingine itakayofanikisha upatikanaji wa fedha hizo kuwa ni pamoja na kutuma barua za maombi ya michango kwa wadau mbalimbali wa utalii kama asasi za kiserikali na zisizo za kiserikali.

Mikakati mingine ni pamoja na kuandaa chakula cha hisani na kufanya tamasha la kitamaduni la chakula, mavazi na ngoma za asili. Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Mrisho ambaye ni Mwenyekiti wa sherehe hizo, ameagiza kamati hiyo ifungue akaunti maalumu ya sherehe itakayokuwa na wajumbe wawili kutoka sekta ya umma na wengine wawili kutoka sekta binafsi na kuupongeza uamuzi wa kamati kufanyia sherehe hizo karibu na Uwanja wa Ndege wa Nduli kwani utaongeza changamoto katika kuendeleza utalii wa Mkoa wa Iringa. Kulingana na waandaaji, wakati wa sherehe hizo wageni watapata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo mkoani hapa kwa gharama nafuu, pia kutakuwa na maonyesho ya vikundi mbalimbali vya burudani.

Wednesday, May 30, 2012


                                                     IDDI AZAM KIZIMBANI TENANI KUJIBU MASHTAKA YA UFISADI UDA, AJIDHAMINI KWA MALI YA SH8 BILIONI BADALA YA SH500 MILIONI ILIYOTAKIWA  
Tausi Ally na James Magai MWENYEKITI wa Bodi ya Shirika la Usafiri  Dar es Salaam (Uda) Ltd, Iddi Simba, jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka manane, likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka na kulisababishia shirika hilo hasara ya Sh2.4 bilioni.Mbali na Simba ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, washtakiwa wengine ni Meneja Mkuu wa Uda, Victor Milanzi na Mkurugenzi wake Salim Mwaking’inda ambaye pia aliwahi kuwa Diwani wa Kata ya Sinza (CCM).

Baada ya Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Benny Lincoln kumaliza kuwasomea mashtaka yanayowakabili, aliieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika na wanaomba kesi ipangiwe tarehe ya kutajwa kabla ya kupangiwa  tarehe ya maelezo ya awali. Wakili Said El- Maamry anayemtetea Simba na mwenzake, Alex Mgongolwa waliiomba Mahakama impatie dhamana mteja wao hoja ambayo haikuwa na pingamizi kutoka kwa Lincoln ambaye alisema mashtaka yanayowakabili washtakiwa yanadhaminika.

Ili kujidhamini, Hakimu Mfawidhi, Ilvin Mgeta aliwataka washtakiwa kutoa hati ya nyumba na kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika, kila mmoja wao asaini bondi ya Sh500 milioni.

Baada ya kutolewa kwa masharti hayo, Simba aliwasilisha hati ya nyumba yenye thamani ya Sh8 bilioni na kuridhia wenzake waitumie kupata dhamana.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa hati hiyo ya nyumba ni ya kiwanda cha Kays Hygiene Products Ltd, kilichoko Mikocheni eneo la Viwanda, Plot namba 23, kinachomilikiwa na Simba na mkewe Khadija.

Simba ni Mwenyekiti wa Taasisi ya mikopo kwa Wajasiriamali ya Pride (T) Ltd na Mwenyekiti wa Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam. Akisoma hati ya mashtaka jana Lincoln alidai kuwa  Septemba 2, 2009 Dar es Salaam, Simba na Milanzi  walikula njama ya kuchepusha fedha kinyume na Kifungu cha 29 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 11 ya 2007.

Lincoln alidai kuwa Simba na Milanzi walighushi barua  wakionyesha kuwapo kwa kiwango zaidi cha fedha kwenye akaunti zote za benki za Uda wakati wakijua kuwa si kweli. Aliongeza kuwa siku hiyo hiyo, Simba na Milanzi kwa pamoja, walichepusha Sh320 milioni wakijifanya ni malipo ya awali ya mauzo ya hisa katika shirika hilo fedha ambazo walijipatia kutokana na nyadhifa zao.

Aidha, kati ya Septemba 3, 2009 na Machi 31, 2010, Simba na Milanzi wanadaiwa kujipatia Sh320 milioni kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa Robert Simon Kisena wakijifanya ni sehemu ya malipo ya hisa za Uda. Lincoln alidai kuwa washtakiwa Simba na Mwaking’inda kati ya Septemba 2009 na Februari 2011, wakati wakitekeleza majukumu yao, kwa makusudi walitumia vibaya nafasi zao waliharibu hisa  milioni 7,880,330 zisizotumika za Uda ambalo ni shirika linalomilikiwa kati ya Serikali Kuu na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam zinazokadiriwa  kuwa na thamani ya Sh1,142,643,935  bila kufuata taratibu za zabuni kitendo ambacho ni uvunjwaji wa masharti ya Kanuni ya 63 (1) ya Ununuzi ya umma.

Washtakiwa hao wote kwa pamoja wanadaiwa kuwa  kati ya Septemba 9 na Februari 11, 2011 wakitekeleza majukumu yao, kwa makusudi walitumia vibaya madaraka yao kwa kugawanya hisa 7,880,330  zisizotumika za UDA kitendo ambacho ni uvunjwaji wa masharti ya vifungu vya ushirikiano katika kampuni  na Kifungu cha 74 cha Sheria ya Makampuni Sura ya 212 iliyorekebishwa mwaka 2002.

Mwendesha mashtaka huyo wa Takukuru, alidai kuwa Februari 11, 2011 washtakiwa hao walishindwa kuchukua tahadhari zinazostahili, walimuuzia Simon hisa milioni 7,880,303 zisizotumika za Uda kwa bei ya Sh1,142,643,935  bila kufuata utaratibu wa zabuni ambao ungeweza kutoa nafasi kwa mnunuzi kutoa ofa ya bei inayolingana na thamani ya hisa hizo, jambo ambalo liliisababishia Uda hasara ya Sh2,378,858,878.80.

Tuesday, May 29, 2012

                                                MSAADA WA HARAKA UNAHITAJIKA
       Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa wanawake wilaya ya Njombe (UWT) Scholastika Kevela

Kutokana na mtoto wa kike katika mkoa mpya wa Njombe ameonekana kutumika sana kama YAYA katika mikoa mbalimbali ya Tanzania hususani katika jiji la Dar Es salaam na kunfanya mtoto huyo kuwa na mazingira magumu huku wakiishia kupata shida na kuhangaika huku wakikosa hata nauli ya kurudi makwao pindi wanapohitaji kufanya hivyo.

Watoto hao wamekuwa wakipata mimba za utotoni kutoka kwa baadhi ya waajiri wao huku wengine wakitafutiwa wanaume wakufanya nao ngono huku ujira akichukuwa mwajili wake  na yeye kuambulia maumivu na mateso ya kuingiliwa kinguvu bila lidhaa yake ukilinganisha na umri,na kuwasababishia matatizo ya kiafya huku wengine wakifikia hatua ya kupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa na ugonjwa wa UKIMWI.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa wanawake wilaya ya Njombe (UWT) Silikcholastika Kevela alipokuwa akizungumza na wanahabari ofisini kwake huku akiitaka jamii kuacha tabia ya kuwakandamiza watoto hao na kuwataka wabadilike.

Kevela ameomba msaada wa wanajamii kujitolea katika kupambana na watu wanaoendelea kutoa ajira kwa watoto wadogo wa mkoa huo wakati wanayo nafasi ya kuendelea na masomo kwa mujibu wa fursa zilizopo za kielimu kwa sasa kutokana na sera ya elimu ya chama cha mapinduzi CCM chini ya mwenyekiti wake Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.

Mwenyekiti huyo ameitaka jamii kuwakemea wazazi wanaokuwa na tamaa ya shilingi 20000 kwa mwezi ambayo bado haikidhi mahitaji ya mtoto huyo na badala yake kuishia kudhalilishwa kijinsia.

JE WATANZANIA TUFANYE NINI KUKABILIANA NA HILI ? kevela amesema maneno hayo akiashiria ni swali kwa jamii.

na McDonald Mollel Masse-Njombe
                                                                             SELL

Whater Through YONO AUCTION MART & Co.LTD
for information mail us at info@yonoauctionmart.co.tz

Monday, May 28, 2012

                                                         Umri wa Lulu bado utata

                                                    Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu)           


 Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akiwa amezungukwa na walinzi kwenye Mahakama Kuu Dar es Salaam jana kutokana na tuhuma zinazomkabili za kuhusishwa na kifo cha msanii mwenzake Steven Kanumba

MAWAKILI wa Serikali katika kesi ya mauaji inayomkabili mwigizaji wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’, wamepinga maombi ya mawakili wa mshitakiwa huyo kutaka umri wake uchunguzwe.

Maombi hayo yalipangwa kusikilizwa jana mahakamani hapo mbele ya Jaji Fauz Twaib, lakini kabla ya kusikilizwa, mawakili wa Serikali walidai kuwa na pingamizi la kusikilizwa maombi hayo.

Awali kabla ya pingamizi hilo, mawakili wanaomtetea Lulu waliiomba Mahakama Kuu ichunguze umri wa msanii huyo au kuiamuru Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ifanye hivyo.

Lakini Wakili wa Serikali, Shadrack Kimaro aliiomba Mahakama hiyo isisikilize maombi ya Lulu kwa madai kwamba yaliwasilishwa mahakamani hapo kimakosa, huku pia sheria iliyotumika ina kasoro.

Sheria iliyotumiwa na mawakili wa utetezi ni Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009, kifungu cha 113 inayoruhusu Mahakama kufanya uchunguzi wa umri wa mshitakiwa.

Kimaro alidai kuwa maombi hayo yalikwishatolewa katika Mahakama ya Kisutu na ‘kugonga mwamba’ na kuongeza kuwa mawakili wa utetezi walitakiwa kuukatia rufaa uamuzi huo au kuomba mapitio yake, lakini si kuwasilisha maombi mapya.

Vile vile Kimaro aliyekuwa akisaidiwa na Wakili wa Serikali, Elizabeth Kaganda, alidai kuwa maombi ya pili kwa Mahakama hiyo ya kusitisha kesi ya Kisutu ni batili.

Alidai ubatili huo ni kwa sababu kesi ya Lulu Kisutu haisikilizwi, iko katika hatua ya uchunguzi na sheria inataka kesi kusimama ikiwa katika hatua ya kusikilizwa.

Hata hivyo mawakili wa Lulu, Peter Kibatala, Fulgence Masawe na Kennedy Fungamtama na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) Joaquine De- Melo aliyetambulishwa kama mtazamaji, walipinga.

Mawakili hao walidai kuwa waliwasilisha maombi yao mahakamani hapo kutokana na uamuzi wa Mahakama ya Kisutu uliotamka kama kuna maombi yoyote yawasilishwe katika Mahakama hiyo.

Walidai kuwa Mahakama ya Kisutu ina uwezo wa kutoa uamuzi wa maombi yao kwa mujibu wa sheria na hakuna walipokosea na kuiomba Mahakama ipuuze maombi ya mawakili wa Serikali.

Baada ya kusikiliza maombi hayo, Jaji Twaib alisema ni vema apate muda wa kutoa uamuzi kwa sababu ana safari na kupanga kutoa uamuzi huo Juni 16.

Lulu jana alionekana mchangamfu akiashiria kuanza kuzoea maisha hayo tofauti na siku za awali, alipokuwa mnyonge mahakamani na wakati mwingine akilia.

Lulu anadaiwa kufanya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba. Upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na itatajwa tena Juni 4 mwaka huu.

 
                                                              Zanzibar si Shwari

VURUGU ZASHIKA KASI, DK NCHIMBI, IGP MWEMA WATOA MAAGIZO MAKALI KWA POLISI
 
Waandishi Wetu
VURUGU zilizozuka kuanzia juzi katika maeneo kadhaa ya Mji wa Zanzibar na kudhibitiwa, ziliibuka tena jana baada ya vijana kuchoma matairi ya magari barabarani wakipinga kurejeshwa rumande kwa Mhadhiri wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar (Jumiki), Sheikh Musa Juma Issa.

Awali, hali ya amani ilikuwa imerejea baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema jana kuongoza mkutano uliojumuisha taasisi mbalimbali visiwani Zanzibar kwa lengo la kutafuta suluhu ya machafuko hayo ambayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa mali.

Hata hivyo, muda mfupi baada ya mkutano huo uliomalizika kwa makubaliano ya kurejea kwa amani, vurugu ziliibuka tena.

Vurugu tena

Kurudishwa rumande kwa Sheikh Issa baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana mahakamani na wenzake wengine sita wakituhumiwa kuhusika na vurugu hizo kulichochea vurugu katika maeneo ya Amani na Mwanakeretwe kwa vijana kuchoma matairi na kufunga mitaa.

Vurugu hizo za vijana zilisababisha polisi kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya vijana hao ambao licha ya kupigwa mabomu walizidi kupiga kelele wakilaani Muungano.

Hadi jana jioni, maeneo ya Chumbuni, Amani, Mwembaladu hali ilikuwa bado tete huku polisi wakifunga barabara kwa ajili ya kudhibiti vijana hao.

Nchimbi, Mwema
Katika mkutano wao, Dk Nchimbi na IGP Mwema walikutana na viongozi wa taasisi za Kiislamu Zanzibar, wawakilishi wa Balozi za Marekani, Norway na Uingereza na kujadili masuala kadhaa ya kuleta amani visiwani humo.

Mkutano huo uliofanyika kwenye Makao Makuu ya Polisi Zanzibar uliwashirikisha pia maofisa wa sekta ya utalii.

Katika mkutano huo, Waziri Nchimbi alisema suala la kulinda amani ni la wote na akawataka viongozi wa dini na wanasiasa kuhakikisha Zanzibar inaendelea kuwa na amani.

“Kwa mwaka mmoja na nusu hivi sasa Serikali ya Umoja wa Kitaifa imefanya kazi nzuri na tunawapongeza viongozi wote kwa kazi hiyo; Rais Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wake wa Kwanza Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wake wa Pili, Balozi Seif Ali Idd, sasa tusiwavunje moyo,” alisema Nchimbi.

Alisema kuendelea kwa vurugu Zanzibar ni kuonyesha viongozi hao wameshindwa kazi jambo ambalo si sahihi na kwamba vurugu zinaweza kusababisha watalii kuondoka na hasa kwa kuzingatia msimu wa utalii unakaribia.

Nchimbi alisema ujio wake Zanzibar, ulilenga katika mambo matatu muhimu... “Kuwahakikishia Wazanzibari wote kuwa Jeshi la Polisi ni lao na litaendelea kuwalinda na kuwaeleza kuwa viongozi wote wa dini na siasa wana jukumu kubwa la kusaidia kujenga mazingira ya utulivu na amani Zanzibar.”

Aliliagiza jeshi hilo kuwatafuta na kuwachukulia hatua za kisheria watu wote waliohusika kufanya vurugu hizo ili haki itendeke.

Kwa upande wake, IGP Mwema aliahidi kushirikiana na viongozi wa taasisi za kidini ili kuendeleza amani na utulivu nchini. Alisema majadiliano na mazungumzo ni muhimu katika kuimarisha amani na kutatua migogoro iliyokuwapo akiahidi kuendelea kubaki Zanzibar.

Taasisi za dini
Kwa upande wake, kiongozi wa Umoja wa Kiislamu wa Elimu, Uchumi na Maendeleo (UKUEM), Dk Mohammed Hafidh Khalfan alilitaka Jeshi la Polisi kuepuka matumizi ya nguvu kubwa wakati wanapotekeleza majukumu yao.

Alisema taasisi yake pamoja na nyingine za Kiislamu zitatumia juhudi na busara za kuwafanya waumini wake waepuke vitendo vya fujo, kwani vinatoa fursa kwa wahalifu kufanya vitendo viovu.

Hata hivyo, katika kikao hicho Jumiki hawakushirikishwa na hivyo Dk Hafidh kushauri kuwa katika kikao hicho sauti za kundi hilo ni muhimu kusikika kwani baadhi ya mambo wangeweza kuyatolea maelezo.

Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (Jumaza), Sheikh Muhidin Zubeir Muhidin ambaye alifanya juhudi za kuwasiliana na polisi na taasisi nyingine katika kutafuta suluhu za machafuko hayo aliahidi kuendelea na ushirikiano na wadau wote wa amani nchini.

“Sote tuna jukumu la kuhakikisha hali ya amani inarudi Zanzibar na Uislamu hautoi nafasi kwa kufanya uharibifu wala kumdhuru mtu,” alisema Sheikh Muhidin.

Mkurugenzi wa Utalii Zanzibar, Ali Khalil Mirza alisema sekta ya utalii inachangia pato kubwa la taifa kwa zaidi ya asilimia 75, inaweza kutetereka iwapo hali ya utulivu itatoweka visiwani humo na kushauri ushirikiano zaidi kati ya taasisi zote na wadau ili kuimarisha hali ya utulivu.

Marekani yajitosa

Ubalozi wa Marekani nchini umezitaka pande zote inazohusika kufanya kazi pamoja na kuhakikisha amani inapatikana visiwani humo.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt ilisema wanajua umuhimu wa mijadala ya kitaifa lakini ni muhimu pande zote zikitumia demokrasia na amani.

“Vurugu hizo zilizotokea kwa siku mbili zilizopita, zinachafua heshima ya Zanzibar ambacho ni kisiwa cha kwanza chenye amani ambacho kilifanya uchaguzi wenye mafanikio ulioleta Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” alisema.

Alisema ni muhimu kulinda amani ya Zanzibar ambayo inaruhusu watalii na maendeleo ambayo ni muhimu kwa Wazanzibari na wageni kwa pamoja.

“Tunataka kila mmoja kulinda maisha na mali za watu wasiokuwa na hatia,” ilisema taarifa hiyo.

Kauli za mawaziri
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki alisema vurugu zinazoendelea visiwani Zanzibar, haziwezi kuzuia shughuli za Tume ya Katiba.
Alisema vyombo vya usalama vitahakikisha vinawakamata na kuwashughulikia wale wote waliohusika katika vurugu hizo.
Kairuki alisema mchakato mzima wa uanzishwaji wa tume hiyo ulifuata sheria na hakuna Katiba iliyovunjwa.
Wakati Kairuki akieleza hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu Hassan alisema hata kama kuna wananchi ambao hawataki Muungano, wanachotakiwa kufanya ni kutoa maoni kwa Tume ya Katiba.
“Wasubiri Tume ya Katiba itakapokuwa ikikusanya maoni ya wananchi waseme kuwa hawautaki Muungano lakini, si vinginevyo,” alisema.
Waziri huyo ambaye alionekana kutotaka kulizungumzia kwa kina suala hilo alihoji iweje aulizwe yeye. Alipoelezwa kuwa yeye ndio waziri anayehusika na masuala ya muungano alisema, “Wasubiri tu.
Kiongozi wa Kanisa
Akizungumzia vuguru hizo, Makamu Mwenyekiti wa Kanisa  Katoliki Parokia ya Mpendae, Geogre Suna alisema vijana hao walivamia kanisa hilo mnamo saa 8:15 kwa kufunga barabara na kisha kuingia ndani na kuanza kuchoma moto mabenchi ya kukalia waumini.

“Baada ya vijana kufika kanisani hapa mlinzi pamoja na fundi waliamua kukimbia kuokoa maisha yao, ndipo wakaanza kuchoma moto, kanisani na kuvunja vioo katika nyumba ya paroko,” alisema.

Katika eneo la Magomeni, vijana hao walivamia kiwanda cha mbao na kukichoma moto na kuchoma matairi na kuweka mawe makubwa barabarani hali iliyosababisha polisi kuwafukuza kwa kutupa mabomu mengi ya machozi pamoja na kupiga risasi.

Mtwara wanena

Wakazi wa Wilaya ya Tandahimba, Mtwara wamesema ili kumaliza kero za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni vyema kwa Katiba mpya ikafuta Zanzibar ili nchi hizo zitambulike kwa Tanzania bara na Tanzania Visiwani.
Wakichangia mada katika mdahalo wa kuwajengea uwezo na kuhamasisha wananchi wa wilaya hiyo kujitokeza kutoa maoni pindi Tume ya Katiba Mpya itakapofika wilayani humo, uliofanyika mjini Tandahimba mwishoni mwa wiki wananchi hao walisema ni wakati sasa kwa Katiba kumaliza kero hizo.

“Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kupata jina moja la Tanzania, iweje leo kuwepo Zanzibar? Hapa kunachotakiwa kuwapo ni Tanzania Bara na Tanzania Visiwani. Zanzibar na Tanganyika tulishaziua kwa kuunda Muungano,” alisema Gebra Msuya mkazi wa Tandahimba.
                                                           AJALI YAUA IRINGA

Askari wa Kikosi cha Usalama barabarani mjini Iringa wakiwa wamebeba moja kati ya maiti za ajali ya Taxi na Fuso iliyotokea eneo la kituo cha Mafuta Eso kwenye barabara kuu ya Iringa -MbeyaFuso yenye namba za usajili T897 AQS baada ya kugongana uso kwa uso na Taxi.
Ajali mbaya imetokea mjini Iringa asubuhi hii na kusababisha vifo vya watu watatu papo hapo baada ya Fuso kugongana uso kwa uso na Taxi.

Mashuhuda waliozungumza na mtandao wa http://wwwmjasiliamali.blogspot.com/ wamedai kuwa Taxi hiyo yenye namba za usajili T620 ANE ilikuwa ikitokea Ndiuka ikiwapeleka wafanyakazi wa barabara katika eneo la Tanangozi ambako ujenzi wa barabara kuu ya Iringa -Mbeya unaendelea .

Hata hivyo kabla ya kufika katika eneo hilo la kituo cha mafuta cha Eso dereva wa Taxi hiyo ambaye alikuwa akitaka kulipita gari jingine lililokuwa mbele yake alishindwa kulipita gari hilo baada ya kukutana uso kwa uso na Fuso yenye namba za usajili T897 AQS ambalo lilikuwa limesheheni magunia ya mpunga.
Hivyo kutokana na mwendo kasi ambao Fuso hilo lilikuwa likienda nao na mwendo kasi wa Taxi hiyo uwezekano wa kukwepana ulishindikana na hivyo kupelekea Fuso hilo kuigonga Taxi na kuipitia kwa juu na kupelekea vifo vya abiria wawili na dereva wa Taxi hiyo papo hapo .

KANISA LILILOCHOMWA MOTO ZANZIBAR
Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) liliopo mtaa wa Kariakoo mjini Unguja, Zanzibar likiwa limechomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Mei 27.
                                MUUNGANO ? AU MUUNGURUMO ?

                   MAKANISA YACHOMWA, WABARA WATAKIWA KUONDOKA

 Moto ukiwaka katikati ya mtaa mjini Zanzibar jana baada ya vurugu za wanaharakati kupinga muungano na kudai Zanzibar ijitawale. 


ZANZIBAR imechafuka. Baada ya kuwapo kwa amani kwa takribani mwaka mmoja tangu kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, vurugu na hali ya wasiwasi zimeibuka tena baada ya wanaharakati wa Kiislam kufanya maandamano kutaka uhuru wa visiwa hivyo.
Zanzibar ilijikuta katika hali tete kiusalama tangu mwaka 1995 baadaya kutangazwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Rais, ambayo Chama cha Mapinduzi (CCM) kiilibuka kidedea na Chama cha Wananchi (CUF) kupinga, lakini uhasama huo ulizikwa Julai 31 mwaka 2010, baada ya kura ya maoni ya kuunda Serikali hiyo ya umoja wa kitaifa.

Lakini kuanzia juzi usiku hadi jana jioni mji wa Unguja na viunga vyake ulitikiswa na mabomu ya kutoa machozi ambayo polisi waliyatumia kutawanya mamia ya wanaharakati hao wa Kiislam wakiongozwa na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI).

Mabomu ya machozi yalipigwa mfululizo juzi usiku na kuendelea kutwa nzima jana, hivyo kuathiri shughuli za biashara, ibada katika makanisa mbalimbali na kusababisha hofu kwa wananchi.

Kwa muda wa saa takriban mbili hivi kati ya saa 3:00 na saa 5:00 asubuhi, helkopta ya polisi ilikuwa ikipasua anga la Zanzibar ambalo lilikuwa limetandwa na moshi uliotokana na mabomu ya machozi pia uchomaji wa matairi ya magari.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa aliwaambia waandishi wa habari kuwa wafuasi hao wamefanya uharibifu mkubwa ikiwa pamoja na kuchoma moto makanisa mawili na kwamba, watu saba akiwamo Imamu wa Msikiti wa Bizeredi, Maalim Mussa Juma wanaotuhumiwa na matukio hayo wamekamatwa na jeshi hilo.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Askofu Dickoson Maganga alisema watu wasiojulikana walivamia kanisa lao eneo la Kariakoo Mjini Zanzibar mnamo saa 4.30 usiku na kuvunja ukuta, kuchoma viti vya plasitiki pamoja na gari yake.

Chanzo cha vurugu hizo kinatajwa kuwa ni wanaharakati hao juzi kufanya mkusanyiko na maandamano makubwa ya kushtukiza ambayo yalizistua mamlaka za usalama visiwani humo, lakini baada ya kutawanyika jioni baadhi ya viongozi wa maandamano hayo walitiwa mbaroni.

Baada ya kukamatwa kwao, wafuasi wao walikusanyika makao makuu ya polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Madema, kushinikiza kutolewa kwa viongozi hao wanaoshikiliwa kituoni hapo.

Habari zaidi zinasema kutokana na hali ilivyo, askari polisi walitarajiwa kuongezwa visiwani humo, ili kusaidia kuimarisha hali ya usalama pia kuwadhibiti wahalifu ambao walikuwa wameanza kuelekea nje ya maeneo ya mji.

Tayari kuna taarifa kuwa askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutoka Tanzania bara jana mchana walingia Zanzibar kwa ajili ya kuongeza ulizi katika mji wa Unguja.

Hata hivyo, katika hali ya kushangaza hakuna kiongozi yoyote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) aliyetoa kauli kuhusu hali hiyo.

Kauli ya Polisi
Kamishna Mussa alisema jeshi lake litaendelea kuwasaka na kuwatia mikononi wote waliopanga fujo hizo pamoja na viongozi wote wa JUMIKI.

“Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar ndio iliyohusika na kuwachochea vijana kukusanyika na kufanya uharibifu ikiwemo kuchoma moto gari, kupanga mawe barabarani na kufanya hujuma mbalimbali kinyume cha sheria. Tutaendelea kuwasaka kwa gharama zote,” aliapa Kamishna Mussa.

Alifafanua kwamba kwa sasa mikusanyiko yote ya mihadhara ya kidini na vyama vya siasa, lazima ipate kibali cha polisi vyinginevyo jeshi lake litatumia nguvu za ziada kutawanya mikusanyiko hiyo ili kulinda sheria za nchi, amani na utulivu.

Hata hivyo, kamishna huyo wa polisi alijizuia kuhusisha harakati za Uamsho na chama cha siasa wala kutaja majina ya viongozi ambao tayari wanashikiliwa na jeshi lake.

“Mpaka sasa hivi sina majina yao kwa jumla, lakini tumewakamata viongozi wa Uamsho na tunatendelea kuwasaka lakini jina moja tu ndio ninalo ambalo ni Mussa Abdallah Juma,” alisema Kamishna huyo.

Hali bado tete
Wakati jeshi la polisi litoa onyo hilo, hali ya usalama ilionekana kuwa bado tete huku maeneo kadhaa ya Mji wa Zanzibar hasa Darajani na Michenzani ambako muda wote ni sehemu zenye harakati nyingi za biashara, jana zilikuwa zimebakia bila pilikapilika kutokana na askari waliojihami kufanya doria katika mitaa yote na kulipua mabomu kila penye kikundi cha watu waliokusanyika wakinywa kahawa.

Mitaa hiyo ilikuwa imechafuliwa kwa mawe, matofali na magogo yaliowekwa barabarani ili kuziba njia kwa ajili kuzuia magari yasipite huku mipira ya magari ikiwashwa moto na vijana hao.

Kwa upande wake Askofu Maganga akizungumzia uvamizi kisha uhalifu uliofanywa kanisani kwake alisema:
“Nasikitika sana kwa tukio hili ambalo tayari tumeiarifu polisi ambao jana (juzi), usiku walifika hapa wakishirikiana na kikosi cha kuzima moto na kufanikiwa kuuzima moto huo ambao kwa habati nzuri haujaathiri paa la kanisa letu,” alishukuru kiongozi huyo.

Alisema kundi la watu ambalo lilikuwa likitoa maneno ya kashfa na kutishia maisha ya waumini waliokuwa wakifanya ibada usiku huo, lilikatisha ibada hiyo pamoja na kusababisha uharibifu wa mali ya kanisa hilo yenye thamani ya zaidi ya Sh 100 millioni.

Kauli ya JUMIKI
Kutokana na hali hiyo, jumuiya hiyo jana ilitoa taarifa yake kwa vyombo vya habari ikikanusha kuhusika na kuchochea watu kuchoma kanisa wala kuharibu mali za watu.

Hata hivyo, Katibu wa Jumuiya hiyo, Abdallah Said alisema katika taarifa hiyo kwamba jeshi la polisi linapaswa kubeba lawama kwa yote yaliotokea kutokana na kuvunja sheria na kuwakamata viongozi bila ya utaratibu wa busara.

“Uislamu ni dini ya amani na inahimiza ushirikiano na utulivu na hatuwezi kuwatuma watu kwenda kuvunja makanisa na kuharibu mali, kwa sababu ndani ya imani zetu tunajua hilo ni kosa na jambo ambalo halifai katika maamrisho ya dini yetu,” alisema Sheikh Abdallah.

Taarifa hiyo ilisema pia kwamba jumuiya hiyo imekuwa wazi katika kudai maslahi ya Zanzibar na sio vinginevyo na kuahidi kufanya hivyo kwa njia za amani, na iwapo watakuwa wamekosea basi wapo tayari kufikishwa katika vyombo vya sheria.

“Ni lazima polisi wajue kwamba tupo tayari kufanya kazi kwa misingi ya kisheria na hata kwa kujisalimisha tupo tayari, lakini ukamataji bila kufuata busara na sheria haukubaliki. Tunachokitaka ni kura ya maoni haraka na hilo tutaendelea kulidai,” alisisitiza katibu huyo wa JUMIKI.

Wakati viongozi wa Uamsho wakiendelea kutafutwa na jeshi la polisi, nyumba ya kiongozi aliyeongoza maandamano juzi Sheikh Farid Hadi Ahmed inadaiwa kuvunjwa milango usiku wa manane alipokuwa akiswakwa jeshi hilo.

Hata hivyo, taarifa hizo hazikuthibitishwa iwapo ni polisi waliofanya kitendo hicho au la, wanafamilia wanasema waligongewa milango na kutakiwa wafungue baada ya kutofungua walisikia kishindo kikubwa cha kusukumwa milango katika eneo la Mbuyuni Mjini Unguja.

Vijana katika mitaa ya Zanzibar jana walionekana wakiwa na hamasa kubwa wakidai kuendelea kuungana na viongozi wao kudai haki ya Zanzibar, pamoja na kutaka Zanzibar huru kutoka ndani ya mikono ya Muungano.

“Sisi tunachokitaka Zanzibar yetu watupige mabomu, watuue, watukamate lakini tunataka Zanzibar yetu na hatusikii lolote,” walisikika baadhi ya vijana.

Hada jana jioni vurugu katika badhi ya maeneo hususan Kwelekwe na njia ya Baa ya Amani zilikuwa zikiendelea na gari moja lilichomwa moto karibu na ofisi ya CCM.

Matukio kabla
Zanzibar imekuwa ikitawaliwa na matukio ya ghasia ambayo licha ya mihadhara hiyo ya Kiislam ilikuwa ni uhasama wa kisiasa kati ya vyama vikuu vya CUF na CCM, hatua ambayo iliwahi kusababisha mauaji ya Januari 27, mwaka 2001.

Lakini, uhasama huo wa kisiasa ambao ni wa kihistoria ulizikwa baada ya kura hiyo ya maoni na uchaguzi mkuu wa 2010 hatua ambayo imemfanya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa SMZ huku baadhi ya mawaziri pia wakitoka katika chama hicho.

Hata hivyo, wanaharakati hao wa Kiislam wameanza upya kuilipua Zanzibar wakishinikiza visiwa hivyo viwe taifa huru kwa kujitenga katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Zitto ataka tume ya uchunguzi
Katika hatua nyingine Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amemtaka Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein aunde kikosi kazi maalum kwa ajili ya kudhibiti
vurugu hizo na kuanza mazungumzo na pande zote kwa kuwa, "Hiki sio kitendo cha kudharau
kabisa."

Alifafanua kwamba waliochoma nyumba za ibada wasakwe na kufikishwa mbele ya sheria mara
moja na kuongeza, "Tusiruhusu hata kidogo wapuuzi wachache kutuingiza katika vurugu za
kidini ili kufikia malengo yao ya kisiasa."

mwisho
Ufugaji wa kuku ni njia ya kuondokana na umasikini

WANANCHI mkoani Mkoa mpya wa Njombe wametakiwa kukataa umasikini kwa kubuni mbinu mbalimbali ambazo zinaweza kuongeza vipato vya familia zao ikiwemo ufugaji wa kuku.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wilaya ya Njombe katika mkoa mpya wa Njombe, Scholastika Kevela wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo. Alisema kuwa, kila kaya ifuge wastani wa kuku watano kwa ajili ya mikakati ya maendeleo kutokana na ukweli kuwa bei ya kuku imeongezeka na kufikia Sh 10,000 kwa kuku moja.

Kevela alisema kuwa wakati sasa umefika kwa wananchi kuachana na dhana kuwa wao ni masikini na badala yake kuwa wabunifu ili kuweza kujiletea maendeleo kuanzia ngazi ya familia. “Wapeni kuku majina, ada, dawati, sare za shule, maendeleo na mkitaka kuku wa kula mwambieni baba atafute kuku wa nyama ndiye atakayechinjwa,” alisema kevela

Alisema kuwa, wananchi kama watafuga kuku na kuwauza kwa malengo yaliyokusudiwa hawatakuwa na shida ya kupata ada kwa ajili ya kulipia karo za watoto wao, kwani wana kuku wengi lakini hawana mipango ya jinsi kuku hao watakavyoweza kuwasaidia pindi wanapouzwa.

Pia Bi.Kevela  aliwataka wananchi hao kupanda miti ili kuwezesha Mkoa wa Njombe kuwa wa kijani. Alisema kuwa, kila nyumba iwe na miti mitano ikiwemo ya matunda ili kuweza kuhakikisha upandaji wa miti unapewa kipaumbele. Alisema kuwa, kama wananchi watazingatia kupanda miti na kuitunza basi kutakuwa na mabadiliko makubwa na Njombe itakuwa ya kijani.

Mwenyekiti huyo aliwataka viongozi wa dini kutumika kupaza sauti za watoto kwa mara nyingi wanabeba uhalisia wa mambo yanayodhihirika kuwa hawapati nafasi ya kusema.
WOMEN AND DEVELOPMENT

By Mcdonald Mollel Masse-Dsm


''In efforts to enhance entrepreneurial capacity amongst Njombe Region womens,Ms Skolastica is vigilantly working towards imparting entrepreneurial skills and advising them on ways to solve emerging hurdles and problems"

With passion of fighting against any oppression against girls and women in the society, Ms Scholastica Kevela is determined to ensure that one day she becomes a high government profile and policy maker in the country.

Having served as Chama Cha Mapinduzi (CCM) Women’s Wing Chairperson for Njombe District since 2008 Ms Scholastica is certain that she was born a leader and would continue to pursue this noble task for the development of women, men and children of this nation.

She stays awake with her dreams, and is determined to fight tooth and nail to ensure set goals are achieved. She believes that women empowerment was vital in attaining national development.

Born in 1967 in Njombe District, Iringa Region, Ms Scholastica completed her primary education at Madaba Primary school in 1983 before joining Songea Girls’ Secondary School the following year and completed in 1987.

After completing form four, she joined the Tanzania Post Corporation in 1989 as Post Officer at Njombe, a post she held for nine years. While serving as a Post Officer in 1994 she also attended a one year certificate course in storekeeping.

The road to success seemed to be rough but she held on, and in 2001 she joined London Metropolitan University where she pursued both an international diploma and advanced diploma in computer studies.

With Information Technologies (IT) subject proving to be quite difficult to most people especially women, this was contrary to Ms Scholastica. She devoted her time and resources pursuing it having in mind that few years down the road everything would have gone digital.

What a life on earth without IT knowledge? Probably this is another thing that forced her to be a great player in this field. Advanced diploma she was conferred did not satisfy her in education ladder. Going back to school to hunt for a bachelor’s degree was the only solution to make her more proficient in IT field.

In 2005, Ms Scholastica was enrolled at the same university for Bachelor of Science in Information System and a year later she was conferred a degree.

With vision of becoming multipurpose and skilful in many academic fields, she is at the meantime pursuing Master’s Degree in Business Administration (MBA) at the Open University of Tanzania (OUT).

Politics being part and parcel of her life and not a dirty game as comically referred to by others, Ms Scholastica since her childhood admired female politicians and was determined to one day climb to the podium and address people.

But what gave her a momentum later in adult life, was her husband’s aspiration in politics. Her husband Mr Yono Kevela had served as an MP for (Njombe-West) hence gave her a chance of seeing politics at home the interested to practice that grew much stronger.

She explains that from primary school through the education ladder, she was elected to hold various leadership positions in the classroom as monitor and later a prefect. At college she was school commander, and at various levels she served as a chairperson for various religious and non religious associations.

The year 2008 was the cornerstone for her politics journey although she describes her attainment as still like water drop in the ocean. She is optimistic that in a near future she will outshine in the field, by not only being a high profile leader but also an activist in women’s right movement.

“My passion for serving the society was accelerated when I was just an ordinary entrepreneur. It was at the course of my involvement in this entrepreneurship when I learned on the best way one can help women and girls fight for their rights, establish income generating activities and generally empower them economically,” she says.

She adds that “Like for ages Iringa Region has been the centre for fetching housemaids who work in Dar es Salaam and other big towns for meagre wages. Coming from the same area, this really disheartens me as among other things, it denied them their basic rights especially to education.”

She said she has started addressing this by educating girls and parents in the area on the importance of education to the children, and their rights in relation to minimum wage that one can be paid.

Ms Scholastica believes that girls like other human beings deserve all basic rights including education, as it is best put that educating a boy is to educate an individual but educating a girl is to educate the entire nation.

According to Ms Scholastica, attention to girls education was vital, not only for the development of the country, but to fulfil the right of every child to education hence the need of ensuring that a big number of girls attend school as would do boys.

Ms Scholastica seeming to be impressed with efforts being made by the government in girls education, particularly on increasing ward secondary schools, she says that such move were laudable and worth praising. The efforts, she add, has greatly helped to reduce the malady of street children especially girls who had in several time fell victims of rape and other gender-based violence.

As a CCM Women Wing Chairperson for Njombe district, Ms Scholastica has been in fore front in ensuring that her dreams of helping women and girls were making headway.
“I have managed to acquire about 30 hectares of land at Itandura Village in a newly-established Wanging’ombe District. The land would be used to build hostels for girls who have been subjected to gender based violence so that they can regain their humanity and pursue normal life,” she said.

In efforts to enhance entrepreneurial capacity amongst Njombe District women, Ms Scholastica is vigilantly working towards imparting entrepreneurial skills and advising them on ways to solve emerging hurdles and problems.

“Empowering women especially in economic aspect is essential, even President Kikwete has been encouraging women to initiate various income generating activities to improve their welfare and that of their families, she stressed.

She said she has decided to start influencing women in Njombe to adopt local chicken raring projects which she said was easy and paid well.

Ms Scholastica welcome other people and well wishers to help women in their localities with view to empowering them economically and subsequently develop the nation.

Currently she serves as Managing Director of Yono Auction Mart &Co. Ltd, Managing Director of Shola General Enterprises and Chaiperson of Women Entrepreneurship Development Forum (W.E.D.F).

Ms Scholastica, a mother of four children calls for women from all walk of life to build confidence and establishe income generating activities assuring them that such efforts always pay.

She is much thankful to her husband Mr Yono Kevela and his children for supporting her in every achievement she has recorded saying without their understanding, much of her goals would not have been met. And having in mind she still got a way to go in realising her leadership dreams, to her sky is the limit.

SIASA

Shibuda: Hakuna chama kama CCM


MBUNGE wa Maswa Mashariki, John Shibuda (Chadema) ameibuka na kusema kuwa kama angekuwa na uwezo, angehakikisha kuwa chama chenye kauli za uchochezi kinashikishwa adabu na kwamba hadi sasa hajaona chama chenye nguvu mithili ya CCM.

Amekifananisha chama hicho tawala kuwa na nguvu sawa na mngurumo wa ndege ya kivita (Airforce). Alisema kuwa, mfumo wa sasa wa vyama vingi umezaa hasira kwa sababu CCM inataka kutawala, ilihali wapinzani nao wanaitaka nchi ili waitawale.

Shibuda aliyasema hayo jana, alipokuwa akitoa mada ya Demokrasia na Siasa wakati wa mafunzo elekezi ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya yanayoendelea hapa. Alikuwa akiwasilisha mada hiyo iliyoandaliwa na Mpango wa Kutathimini Utawala Bora Afrika (APRM).

Alisema kuwa gazeti moja la kila wiki mapema wiki hii lilikuwa na habari iliyokuwa na maneno `CCM yakaribia kuaga Ikulu’, lakini akasema kamwe hajawahi kuona chama chenye mngurumo wa Airforce kuweza kuizidi CCM na kushika nchi.

“Ningekuwa na uwezo mara ninaposikia kuna uchochezi sitamkamata mtu aliyetoa maneno ya uchochezi, bali nitakipiga faini chama chake kwa lengo la kuhakikisha kuwa kinabadili lugha zake, kwani chama chenye uchochezi kikipigwa faini mara nyingi kitakuwa na nguvu tena?” alihoji Shibuda.

Alisema kuwa, fitna mara nyingi zimekuwa malighafi za kisiasa kutokana na maneno matamu, lakini APRM ni chujio na kuwa mfumo wa vyama vingi huzaa wawindaji.

“Kiongozi anayekaa ofisini hawezi kujua kiu ya wananchi wake, ni lazima kujisahihisha na kujitathimini, kwani Serikali na siasa ni kama mapacha, lakini cha muhimu ni kujiuliza vipi tutalinda mitaji yetu? Kwani kuna vishawishi vya kuacha mema na kukumbatia upumbavu, lakini matunda matamu hutambulishwa na mbegu za kuzaa matunda matamu,” alisema.

Aliongeza kuwa, siasa za sasa zimejaa unafiki mfano wa malezi ya machokoraa (watoto wasio na makazi maalumu) ambayo hayakupata malezi ya baba na mama.

“Mfumo wa vyama vingi unazaa hasira kwa sababu tunataka kuwakomoa wapinzani na CCM inasema inataka kuwamaliza wapinzani, lakini ukimaliza mazalia ya mbu malaria haitakuwepo,” alisema.

Alisema kuwa, Rais Jakaya Kikwete ni mwanasiasa na bila siasa hakuna kilainishi cha kuongoza na kutawala .

“Wakoloni walitumia machifu wa Kisukuma kutawala, wanaweza kukushangilia ukajua wanafurahia kumbe wanatafuta mwanya wa kukuadhibu,” alisema Shibuda. Alisema kuwa mwanzoni alikuwa CCM na sasa yuko upinzani, hivyo ana taswira ya nchi inakoelekea.

Aliongeza: “Najiuliza, naacha urithi gani kwa wadogo zangu waliochaguliwa kuwa Wakuu wa Wilaya?”.

Shibuda aliwataka viongozi wa Serikali kuhakikisha wanatunza vizuri historia ya nchi akisisitiza historia inahifadhiwa, lakini kama mtoto ni chokoraa, hatakuwa na uwezo wa kutunza historia.

Aliongeza kuwa, siasa ni daraja la maoni kwa ajili ya kuongoza umma na kila chama kimekuwa kikishindana kwa lengo la kuhakikisha kuwa kinashinda uongozi.

Aidha, Shibuda alitumia fursa hiyo kukishukuru CCM kutokana na uelewa wake, huku akisema hataki chama hicho kife, kama ambavyo pia hataki Chadema ife.

Mafunzo hayo elekezi yanayofanyika mjini Dodoma yanahudhuriwa na Wakuu wa Mikoa 24, Makatibu Tawala wa Mikoa 25 na Wakuu wa Wilaya 133.
MAENDELEO YA WILAYA YA NJOMBE
Na mwandishi wetu-Njombe

UWT yatoa masaada wa baiskeli
UMOJA wa Wanawake (UWT), Wilaya ya Njombe umetoa msaada wa baiskeli kwa wanawake wawili wenye ulemavu wilayani humo ambao pia ni wajane ili kuwasaidia katika harakati za maisha.

Msaada huo una thamani ya Sh1.5 milioni, ulitolewa na
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Njombe, Scholastica Kevela katika Kata ya Mjimwema iliyopo Njombe Mjini.

Walemavu waliokabidhiwa baiskeli hizo ni Janeth Mfugale na Anna Mwagosela kutoka Kata za Igamba na Igominyi.

Akikabidhi msaada huo jana, Mwenyekiti wa UWT, Mkoa wa Iringa, Zainabu Mwamwindi alisema msadaa huo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2010/2015 ili kustawisha maisha ya watu wa makundi maalumu wakiwamo watu wenye ulemavu.

“Najisikia kuwa na furaha kubwa leo baada ya kuwakabidhi hawa wanawake baiskeli hizi maana maisha waliyokuwa wanaishi ni ya taabu sana kutokana na kutembea kwa kusota huku wakiwa na familia zinazowategemea,”alisema Mwamwindi.

Alisema UWT Mkoa wa Iringa inaipongeza UWT Wilaya ya Njombe kwa kuona umuhimu wa kuwasaidua wanawake hao na alimpongeza Mwenyekiti wa UWT wilaya hiyo kwa kutimiza ahadi ya kuwasaidia wanawake aliyoitoa alipokuwa anawania uongozi wa umoja huo.

Kwa upande wake Kevela alisema ni wajibu wa serikali na Watanzania wote
kuwasaidia watu wanaoishi katika mazingira magumu kama watu wenye ulemavu ili kujenga Tanzania yenye upendo, amani na mshikamano.

“Hawa kina mama na ni walemavu, lakini pia ni wajane, leo
najisikia furaha sana kwa kutoa msaada kwao maana niliwaona wakati nikiwa kwenye ziara zangu nikaahidi kuwasaidia ili kuwaondolea mateso waliokuwa wakipata,” alisema Kevela.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Mfugale alisema: “Najisikia vizuri sana leo, nimeishi kwa mateso kwa miaka mingi na hatimaye leo Mungu amesikia kilio changu, nawashukuru sana UWT Mkoa wa Iringa na hasa Mwenyekiti wetu wa Wilaya ya Njombe, kwa kuniondolea mateso haya.”

Naye Mwagosela alisema: “Sina ndugu nimekuwa naishi maisha magumu namshukuru sana Mungu na CCM kwa msaada huu, naomba waendelee na moyo huu.”

Diwani wa Kata ya Idamba, Chabiko Ihenga alisema msaada kwa wanawake hao
utaondoa simanzi na masikitiko yaliyokuwa yanatokana na maisha mgumu nay a tabu waliyokuwa wanaishi walemavu
                                    karibuni tuijenge ilembula kupitia wwwmjasiliamali.blogspot.com
 Mkurugenzi wa YONO AUCTION MART SCHOLASTIKA KEVELA (wa kwanza kushoto) na watenda kazi wa kampuni hiyo katika maonyesho ya wajasiliamali Mnazi mmoja.
 Mbunge mstaafu wa jimbo la Njombe Magharibi Stanley Yono Kevela akiwa amesimama katika kibao cha msitu wa asili wa NYUMBANITU.

SAMAHANI KWA KUKATIKA KATIKA MATANGAZO YETU KWA MUDA TUTAREJEA BAADA YA MUDA MFUPI..........................
MWENYEKITI WA UWT NJOMBE KUKOMBOA WANAWAKE WA MKOA WA NJOMBE

Akizungumza na wanahabari wa mkoani humo mwenyekiti wa umoja huo Scholastika C.Kevela ameahidi kuwasaidia wanawake wa mkoa huo katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujasiliamali.

Amesema kutokana na mkoa huo kuwa na fursa nyingi za uwekezaji na kumilikiwa na wanaume pekee hivyo kuwafanya wanawake kuamini kuwa fursa hiyo ni kwa wanaume pekee huku akiita ni mtazamo hasi na badala yake wabadilike kwa kufanya kazi na kuthubuthubutu.

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Njombe Scholastika Kevela (wa katikati) akizungumza na wanahabari wa mkoa mpya wa Njombe.

Picha na Mcdonald Mollel Masse-Njombe